Hii ni blog ambayo inakupa Taarifa na habari Zote Za Kitaifa na za kimataifa Katika Nyanja Zote za kisiasa, Uchumi, michezo na burudani..

Saturday, August 10, 2024

Maneno ya Gamondi

 “Huu ni mchezo wa fainali, unapaswa kuwa makini sana, nakumbuka vyema mchezo uliopita pale Zanzibar, tayari tunayo picha sahihi tunapaswa kwenda na mbinu gani dhidi ya Azam Fc, niwahakikishie Yanga Sc ni timu imara sana, ukitazama mchezo uliopita Simba walitengeneza nafasi moja tu kwa sababu tulikuwa imara kwenye kila idara.” Kocha Mkuu Miguel Gamondi kuelekea mchezo wa fainali #ngaoyajamiii dhidi ya Azam Fc.


#Yanga_Ya_Master_Gamondi

Wednesday, August 7, 2024

Akamatwa Kwa Kutoa Taarifa ya Uwongo


 JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Amos Lwiza (54) mkazi wa Tegeta Wazo wilaya ya Kinondoni mkoani humo, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuwa binti mkazi wa Yombo Dovya ambaye video zake zilisambaa mitandaoni akibakwa na kulawitiwa na vijana watano kuwa amekutwa tayari kashafariki dunia.

Kamanda Muliro amesema binti huyo anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai hajafa, kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na kwamba uchunguzi wa tukio hilo la kikatili bado unaendelea.


Tuesday, August 6, 2024

Pilato wa Tarehe 8/8/2024

 Mwamuzi Elly Sasii amechaguliwa kuchezesha mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Young Africans Sc dhidi ya Simba Sc itakayopigwa Agosti 8, 2024 katika dimba la Mkapa.


Aidha Mwamuzi Ahmed Arajiga atachezesha mechi ya Azam Fc dhidi ya Coastal Union utakaopigwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar Agosti 8, 2024.