Sunday, September 29, 2024

 WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) imetoa sh milioni 38.2 ili kufungwa kwa mfumo wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dk. Samia Suluhu Hassan mkoani Ruvuma ikiwa ni utekelezaji kwa vitendo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Shule hiyo ya kisasa yenye wanafunzi zaidi ya 540 kwa sasa ipo katika Wilaya ya Namtumbo katika Mkoa wa Ruvuma ilizinduliwa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan Septemba 27.



Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa shule hiyo, Mkurugenzi wa wa Mipango na Utafiti REA, Mhandisi Godfrey Chibulunje amemshukuru Rais kwa kuendelea kutoa fedha zinazowezesha wakala kutekeleza miradi yake mbalimbali kwa wakati ikiwamo miradi ya nishati safi ya kupikia.

“REA tunaendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali pamoja na Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo na katika shule hii tumetoa sh milioni 38.2 kwa ajili ya kufungwa mifumo ya nishati safi ya kupikia tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanatumia kuni kupikia,” amesema Mhandisi Chibulunje.


Mhandisi Chibulunje amesema, REA itahakikisha shule mbalimbali zinafungwa mfumo wa nishati safi wa kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na kuongeza kuwa wakala huo umesaini mikataba ya zaidi ya Sh bilioni 50 kuhakikisha taasisi zinazolisha watu zaidi ya 300 kama magereza na kambi za jeshi zinafungiwa mifumo ya nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma kutoka REA, Martha Chassama amesema wakala umejipanga kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia huku akiendelea kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia

 RAIS SAMIA ATOA TRILIONI SITA KÜTEKELEZA MIRADI CHINI YA TAMISEMI 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imetoa fedha takribani Sh. Trilioni sita tangu Mhe. Rais  Samia Suluhu Hassan aingie madaraka kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI.


Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akitoa salam za Wizara kwenye mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya siku sita ya Rais Samia mkoani Ruvuma uliofanyika kwenye uwanja wa Majimaji  mjini Songea .

 


Amesema “Mhe. Rais fedha ulizotoa zimeenda kila Mkoa, Halmashauri, Tarafa, Kata, Kijiji, Kitongoji na kila mtaa na zimegusa wanawake kwa wanaume, wazee, vijana, watoto na hata walemavu.”


“Hakuna kundi ambalo halijafikiwa na huduma zilizopelekwa kupitia fedha hizo ulizotoa, umegusa maisha ya watanzania, umegusa mioyo yao na umeboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi,”amesema.


Amefafanua miradi iliyotekelezwa kwa kipindi hicho kuwa ni  Hospitali za Wilaya 129 mpya zimejengwa na hospitali Kongwe 50 zimekarabatiwa, Vituo vya Afya 367 vimejengwa, majengo ya kutoa huduma za dharura (EMD) 87 zimejengwa, Majengo ya kutoa huduma za Wagonjwa mahututi 28 yamejengwa, Mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya Oksjen 21 imesimikwa, magari ya kubebea wagonjwa pamoja na usimamizi wa shughuli za Afya  523 yamenunuliwa.


“Kila Halmashauri nchini imepata gari la kubebea wagonjwa pamoja na gari la usimamizi wa shughuli za afya na hapa kwenye Mkoa wa Ruvuma wamepokea magari ya Wagonjwa kwa kila Halmashauri,”amesema


Aidha, amesema kwa upande wa elimu hadi sasa Shule mpya za Sekondari kwa Kata  458 zimejengwa, Shule za Msingi 665 zenye madarasa ya awali na vyumba vya madarasa 50,050 vimejengwa

Saturday, September 14, 2024

 Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Amiri Rashid Matumla a.k.a 'Snake Boy Jr' ametangaza wazii kumtaka ndani ya ulingo bondia kutoka Mabibo King Of Naccoz Camp Mfaume Mfaume a.k.a 'Mapafu ya Mbwa'.


Amiri huyu ni mtoto pekee wa Mzee Rashid Ally Matumla Legendary wa mchezo wa Masumbwii hapa nyumbani anaecheza ngumi kijana huyo ameonyesha niya ya kumtaka bondia Mfaume ili kulipiza kisasi cha mchezo wa Ndondi kwa ndugu yake na kaka ake mkubwa Mohammed Matumla. 


Itakumbukwa Mfaume na Mohammed waliwahii kukutana Tarehe 5/2/2017 kwenye pambano la utangulizi la raundi 8 lililowahii kupigwa Uwanja wa ndani wa Taifa na bondia Mohammed Matumla alipoteza pambano hilo kwa matokeo ya 'K.O' kwenye raundi ya 7 tukio ambalo lililomletea madhara na itilafuu kwenye kichwa chake na kusababisha yeye kuachana na mchezo wa Masumbwii.


Baada ya tukio hilo imepita miaka 7 sasa na kimevumbuliwa kipaji kingine kutoka kwenye familia hiyo ya Matumla familia ambayo ina historia nzuri na mchezo huu wa Masumbwii.


Na kwa mujibu wa mtandao wa Boxrec Amiri ni bondia kinara wa uzani wa Super Welterweight kg 69 hapa nyumbani akishika nafasi ya kwanza kati ya mabondia 26 wanaocheza uzani huo wa kg 69 hapa nyumbani akiwemo bondia Mfaume. 


Ambae kwa sasa rekodi yake ipo Inactive kwenye upande wa nafasi kutokana nakuto kucheza kwa mda mrefu kidogo tangu alivyocheza pambano lake la mwisho mwaka jana dhidi ya bondia Chikondi Makawa raia wa Malawi na kuibuka mshindi kwa matokeo ya point ya majaji wote watatu.


Baada ya sakata hilo baadhii ya wadau wa mchezo wa Ndondi kila mmoja kwa nafasi yake wamekuwa wakitoa maoni yao tofauti tofauti kwenye sakata hilo kwani wapo wanao ona kijana ni wakati wake sahihi wa kucheza na bondia Mfaume Mfaume.


Na kuna wengine wamekuwa na maoni tofauti kwamba kijana huyo huu sii wakati mzuri kwa upande wake kucheza na bondia huyo anahitajika kukuwa na kukomaa kidogo kwa kucheza mapambano kadhaa magumu kabla ya kumvaa bondia Mfaume Mfaume.



Amiri ana Totally Fight's 5, Win's 5, 'KO'S' 2, Lose 0 & Draw 0.


Mfaume ana Totally Fight's 28, Win's 18, 'KO'S' 8, Lose 8 & Draw 2.