Choki Mbabe
Bondia Mtanzania wa uzito wa Feather, Juma Ramadhani Choki, ameibuka na ushindi katika pambano lake la kwanza la raundi ya 32 la mashindano ya kwanza ya Kombe la Dunia la ngumi yalioanza leo mjini Riyadh Saudi Arabia, akimchapa kwa pointi za majaji wote watatu bondia wa Ufilipino Bryx Piala.
Choki anayejulikana zaidi kwa uwezo wake mkubwa wa kurusha makonde hatarishi, amemchapa Bryx Piala kwa pointi za majaji 58 kwa 56, 59 kwa 55 na 59 kwa 55 na kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.
Katika hatua hiyo, Choki atakwenda kuvaana na Hector Munguia Calderon raia wa Mexico ambaye amemchapa kwa TKO raundi ya 6 mpinzani wake Idris Timileyin Gbadamosi.
Hector ana rekodi ya kushinda mapambano 15 akitoka sare pambano moja na kushinda mapambano 9 kwa KO na TKO.
Washindi wa kategori nne za uzito kwa maana ya Featherweight, Super Lightweight, Middleweight na Heavyweight wataondoka na Dola za Marekani 200,000 sawa na zaidi ya Milioni 500 za Tanzania na kupata nafasi ya kuwa washindi wa lazima 'Mandatory Challenger' wa ubingwa wa WBC Silver
No comments:
Post a Comment