Hii ni blog ambayo inakupa Taarifa na habari Zote Za Kitaifa na za kimataifa Katika Nyanja Zote za kisiasa, Uchumi, michezo na burudani..

Monday, October 19, 2015

MABIGWA 5 KATIKA BURUDANI ZA MIELEKA DUNIANI, MWEZI WA 10/205

Kutokana na mechi mbalimbali katika World Wrestling Entertainments (WWE),zinazoendelea huko Marekani ndani ya mwaka huu 2015 katika mashinadano matano ambayo ni.


1. Wwe World Heavyweight Champion, Na bingwa wa Mkanda huu ni Seth Rollins ambapo kama unakumbuka Rollins aliweza kushinda mkanda hu wa Heavyweight pale ambapo Superstar Brock Lesnar na Roman Reings walipokuwa wakipigana na Seth kuingilia mwisho wa machi hiyo lakini kutokana na sheria za mchezo huo Seth aliweza kushinda. 
 
 2.  Intercontinetal Champion, na bingwa wa mkanda huu adi sasa ni Kevin Owens.



3. United State Champion, ambaye bingwa wa mkanda huu ni WWE Superstar John Cena.





4. Tag Team Champion, ambaye bigwa wa mkanda huu ni mpiganaji machachali Koff Kingston, 



5. Divas Champion, na bingwa wa mkanda huu ni mdada ambaye naye ni machachali sana anaitwa Charlotte,  shindano hili ni la wadada.


 Hawa ndiyo mabingwa ambao wanaendelea kushikilia mikanda hiyo yote ya World Wrestling Entertainments.

Saturday, October 10, 2015

Miaka 25 ya Chris Jericho ndani ya WWE




Chris Jericho asherehekea miaka 25 katika michezo ya burudani na ‘ wakanada wenzake’

Chris jeriko ameweza kusherehekea leo tarehe 8 october miaka 25 katika mchezo wa burudani za mieleka (wwe)tangia ajiunge katika michezo hiyo, akiwa katika kusherehekea sherehe hizo Jericho a.k.a Y2J alisindikizwa na pambano la Intecontinetal Champions kati ya Brock Lesnar na The Big Show.
 


Katika sherehe hizo Jeriko alisema “hii inamaanisha kuwa nina marafiki wengi sana hapa ndani ya michezo hii. Lakini ni kitu gani bora zaidi ambacho ninaweza kufurahia usiku huu kuliko miaka yote iliyo pita ?” Jericho aliiambia Wwe .com. vilevile aliendelea kuiambia Wwe.com kuwa “ marafiki zangu ka Don Callis a.ka. wwe the Jacky hakuweza huwa  tangia mwaka 1996 au 1997 na had sasa ni miaka 10 imepita lakini pia rafiki yangu Len Olsen a.k.a “Luscious” hakuweza kuwepo hapa kwahiyo nawaitaji wao safu ya mbele kwasababu hii inamaanisha kitu kwangu”.
Marafiki zake kutoka Canada:

Wwe superstar chris jericho(wa pili kutoka kulia) akiwa na marafiki zake kutoka canada ambao walimsindikza katika sherehe za miaka 25 ya Jericho ndani ya michezo ya burudani za mieleka.

“Ukweli ni kwamba Chris anautajiri wa kutosha leo na hadi kusherehekea sikukuu za miaka 25”alisema Stom ambaye Chris Jericho alimchagua kuwa wa kwanza kuzungumza. “na tunapenda kusema kuwa tunafuraha ya kuweza kushinda mikanda ya NWA na WWE world champions, na Jericho ni mmoja kati ya aliye wapiga The Rock na Steve Austin katika usiku hio “ alisema Stom.

“Sitoweza kupata tena usiku kama huu”
alisema Jericho alipo kuwa akiwashukuli wote walio hudhulia katika sherehe hizo.