Bondia mahiri, mwenye pumzi pindi awapo ulingoni Frances
Cheka anatarajia kuzichapa na mpinzani wake wa jadi Thomas Mashari tarehe 25
mwezi huu huko Mji kasoro bahari Morogoro.
Pambano hilo ambalo litasindikizwa na pambano kati ya Mohamed
Matumla a.k.a Matumla Jr na Mfaume Mfaume a.k.a Master, lakini pambano hili la
kusindikiza litakuwa na upinzani mkubwa kutokana na kwamba Mfaume Mfaume
alikuwa anamtafuta sana Mohamed Matumla, lakini Matumla Jr alikuwa akimkwepa.
\
Mfaume
Mfaume auzungumzia mchezo huo:
Bondia Mfaume, hayupo pichani ambae anashika nafasi ya tatu kwa ubora katika
uzani wa kilo 63 kwa mabondia wa Tanzania wakiongozwa na bondia Twaha Kiduku,
na kufuatiwa na Ibrahim Class a.k.a King Class Mawe. Ameweza kujinadi kuwa
mchezo huo ataumaliza kwa Round tu
Amesema kwanza nashukuru tangia nimeanza mchezo huu nikiwa
chini ya kocha wangu Rama Jah hadi sasa nimepigana mapambano tisa yasiyo ya
Ubingwa na nimeshinda nane na kupoteza moja ambalo nilipigana na Cosmas Cheka.
Hata hivyo Mfaume alijinadi kuwa hadi sasa kuna mabondia
baadhi wananikwepa kama Matumla Jr, na mwingine ni Cosmas Cheka ingawa awali
alinipiga kwa pointi hivyo nawaambia wajipange kwa maana niko vizuri kwa sasa
baada ya kunolew vya kutosha na kocha wangu Rama Jah na ninaaminim nitamchapa
kwa round.
No comments:
Post a Comment