Bondia wa ngumi za kulipwa Tanzania Francis Cheka ameingia
mafichoni kujiandaa kwa pambano lisilo la ubingwa la Round 12 dhidi ya Tomas
Mashali, lililo pangwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu, katika uwanja wa
jamuhuri mjini Morogoro.
Akizungumzia pambano hilo Cheka alisema kwa kuwa Tomas
Mashali ametamba kuwa atampiga kasha atastaafu, yeye ameanza kujifua mapema ili
aweze kumchapa katika round za mwanzo.
Alisema amepania kuweka historia mpya kwa kumtwanga mapema
mpinzani wake na kukata ngebe zake, huku akieleza kuwa kitendo cha kutamba
mpinzani wake kimemuongezea hasira, hivyo atamstaafisha kupigana ngumi mara
baada ya kumuadhibu katika Round tatu za mwanzo.
![]() |
Bondia Tomas Mashali. |
“yeye si anataka
kuachana na masumbwi kwa kuweka historia ya kunipiga, basi nitaingia mafichoni
kwa ajili yake na tutakapo kutana ajiandae kupata kipigo cha historia kutoka
kwangu” alisema Cheka
Tomas Mashali (kushoto) akisaini mkataba dhidi ya pambano lake na Francis Cheka, katikati ni Promota wa ngumi Kaige Siraju. |
Aidha alimaliza kwa kusema ataonyesha vitendo kwenye ulingo
ili aweze kuongeza heshima ya katika medani ya ngumi.
No comments:
Post a Comment