Hii ni blog ambayo inakupa Taarifa na habari Zote Za Kitaifa na za kimataifa Katika Nyanja Zote za kisiasa, Uchumi, michezo na burudani..

Tuesday, November 10, 2015

Vifaa vya Judo kupigwa Mnada





Vifaa vya mchezo wa Judo vilivyotolewa na Shirikisho la mchezo huo Duniani IJF, viko hatarini kupigwa mnada baada ya chama cha Judo Tanzania  JATA, kushindwa kulipia ushuru ili kuvigomboa bandarini.



Akizungumziasakata hilo Katibu mkuu wa JATA, Innocent Malya amesema chama chake kimeshindwa kulipa ushuru ili kuvikomboa vifaa hivyo kutokana na changamoto mbalimbali na hivyo huenda vikapigwa mnada.



Malya alisema wakiamua kuwaambia ukweli JIF, kwamba wameshindwa kulipia ushuru ili vifaa virudishwa viliko toka  huenda waka vipeleka na hicho ndicho kikwazo kingine baada ya selikari kutaka vilipiwe deni wanalo daiwa ambapo IJF, ilisaidia kwa kutoa sh. milioni 3.6, na kilicho baki kilikuwa sh. milioni 9.2 ili viweze kutolewa.
Baadhi ya wanafunzi wa JUDO nchini Tanzania wakionyesha bendera ya Taifa.


Hata hivyom alisema kinacho elekea kutokea kinafanana na kilichowahi kufanyika mwaka 2006, ambapo JIF iltoa vifaa lakini vilikwama bandalini baada ya kukosekana kwa fedha za kulipia ushuru hatua iliyom sababisha vipigwe mnada.


No comments:

Post a Comment