Hii ni blog ambayo inakupa Taarifa na habari Zote Za Kitaifa na za kimataifa Katika Nyanja Zote za kisiasa, Uchumi, michezo na burudani..

Monday, November 2, 2015

Frances Cheka kuzichapa na Thomas Mashali


 Bondia mahiri, mwenye pumzi pindi awapo ulingoni Frances Cheka anatarajia kuzichapa na mpinzani wake wa jadi Thomas Mashari tarehe 25 mwezi huu huko Mji kasoro bahari Morogoro.


Pambano hilo ambalo litasindikizwa na pambano kati ya Mohamed Matumla a.k.a Matumla Jr na Mfaume Mfaume a.k.a Master, lakini pambano hili la kusindikiza litakuwa na upinzani mkubwa kutokana na kwamba Mfaume Mfaume alikuwa anamtafuta sana Mohamed Matumla, lakini Matumla Jr alikuwa akimkwepa.

 \

Mfaume Mfaume auzungumzia mchezo huo:
Bondia Mfaume, hayupo pichani ambae anashika nafasi ya tatu kwa ubora katika uzani wa kilo 63 kwa mabondia wa Tanzania wakiongozwa na bondia Twaha Kiduku, na kufuatiwa na Ibrahim Class a.k.a King Class Mawe. Ameweza kujinadi kuwa mchezo huo ataumaliza kwa Round tu


Amesema kwanza nashukuru tangia nimeanza mchezo huu nikiwa chini ya kocha wangu Rama Jah hadi sasa nimepigana mapambano tisa yasiyo ya Ubingwa na nimeshinda nane na kupoteza moja ambalo nilipigana na Cosmas Cheka.

Hata hivyo Mfaume alijinadi kuwa hadi sasa kuna mabondia baadhi wananikwepa kama Matumla Jr, na mwingine ni Cosmas Cheka ingawa awali alinipiga kwa pointi hivyo nawaambia wajipange kwa maana niko vizuri kwa sasa baada ya kunolew vya kutosha na kocha wangu Rama Jah na ninaaminim nitamchapa kwa round.

No comments:

Post a Comment