Hii ni blog ambayo inakupa Taarifa na habari Zote Za Kitaifa na za kimataifa Katika Nyanja Zote za kisiasa, Uchumi, michezo na burudani..

Saturday, November 14, 2015

Floyd Maywether achafua hali ya hewa huko Miani.





Hii ni sherehe ya kawaida kwake ambapo ilifanyika nyumbani kwake yeye mwenyewe Floyd Mayweather huku akizungukwa na wacheza dansi wa kike, naye akirusha note hewani za pesa, Milionea huyo alionekana kufurahia maisha yake ya kustaafu Ndondi.
Floyd Maywether akiwa Team noney.


Bondia huyo asiye pigika alirusha hewani noti za dola za malekani huku furaha yake ikipambwa na marafiki zake ambao waliuzulia sherehe hiyo huku yeye akisema.
“ni sherehe ya kawaida kwangu saa 11:16 alfajiri maisha yangu ni matamu aliandika katika ukrasa wake wa Instagramjana.

Mtu wangu wa Face2face kama unakumbuka bondia huyo alistaafu Masumbwi baada ya pambano lake lililopita lakni bado anashawishiwa kurejea stejini kumkabiri Andrea B erto, ambaye amepania kuharibu rekodi yake ya Mataji 49-0 mjini Las Vegas hii si mara ya kwanza kwa Mayweather, kuchafua jamii kwa mtindo huo kwani Mwaka jana mwana masumbwi huyo mtata aliwaita madensa hao nyumbani kwake na kuporomosha bonge la Party kwa mtindo huo huo.


Lakini pia mkari huyo wa ndondi amekuwa akijirusha kwa sherehe mbalimbali zisizo za kikomona Team yake ya Pesa (money Team), tangu atangaze kustaafu huku akifika hatua ya kubeba fuko la fedha na kwenda nalo hadi klabu ya usiku ya Miani ya Marekani mwezi uliopita.

Francis Cheka mafichoni kumkabili Tomas Mashali





Bondia wa ngumi za kulipwa Tanzania Francis Cheka ameingia mafichoni kujiandaa kwa pambano lisilo la ubingwa la Round 12 dhidi ya Tomas Mashali, lililo pangwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu, katika uwanja wa jamuhuri mjini Morogoro.
 
Bondia francis Cheka akipewa mafunzo na master wake.
Akizungumzia pambano hilo Cheka alisema kwa kuwa Tomas Mashali ametamba kuwa atampiga kasha atastaafu, yeye ameanza kujifua mapema ili aweze kumchapa katika round za mwanzo.


Alisema amepania kuweka historia mpya kwa kumtwanga mapema mpinzani wake na kukata ngebe zake, huku akieleza kuwa kitendo cha kutamba mpinzani wake kimemuongezea hasira, hivyo atamstaafisha kupigana ngumi mara baada ya kumuadhibu katika Round tatu za mwanzo.
Bondia Tomas Mashali.


 “yeye si anataka kuachana na masumbwi kwa kuweka historia ya kunipiga, basi nitaingia mafichoni kwa ajili yake na tutakapo kutana ajiandae kupata kipigo cha historia kutoka kwangu” alisema Cheka
Tomas Mashali (kushoto) akisaini mkataba dhidi ya pambano lake na Francis Cheka, katikati ni Promota wa ngumi Kaige Siraju.

Aidha alimaliza kwa kusema ataonyesha vitendo kwenye ulingo ili aweze kuongeza heshima ya katika medani ya ngumi.

Wayne Rooney amchapa Kofi bondia wa Mieleka.





Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney amekutana “FACE2FACE” Yaani Uso kwa Uso kwa kumchapa kibao nyota wa Mieleka Wade Barrett, mwenye urefu wa futi sita na nchi saba Mita 2.0066 mbele ya mashabiki katika uwanja wa WWE.

Rooney alifikia uamuzi huo baada ya kukashfiwa na mwanamichezo huyo mbele ya mwanae Kai Rooney, mcheza mieleka huyo Wade Barrett, mwenye urefu wa futi sita na nchi saba (mita 2.0066) alidaiwa kumkosea adabu nyota huyo wa soka England.
Mwanamieleka, wade Barrett (kushoto) akikunja uso baada ya kuchapwa kibao na Mwanasoka Wayne Rooney, (kulia).

 Rooney alieleza kukerwa na kitendo cha Barrett kumkashfu hadharani akitumia kipaza sauti, huku mwana mieleka huyo mzaliwa wa Lancas Hire alitwaa kipaza sauti na kusema.
Mwanasoka wa timu ya Manchester united Wayne Rooney (kushoto) na Mwanamieleka Wade Barrett.

“Mbele yenu kuna watu wawili mnao weza kuwaita mashujaa ni nani zaidi kati ya Wayne Rooney na Manchester united, huku Bennett akimtuhumu Rooney kwa kujiangusha uwanjani wakati wa mechi ya kombe la FA dhidi ya preston North End.

ukitaka video links hapa uone jinsi kilicho tokea baada ya Barrett kuchapwa kibao.
 http://www.wwe.com/videos/king-barrett-hunts-for-wayne-rooney-at-old-trafford- november-10-2015-28193399

Rooney aliudhulia onyesho hilo akiongozana na rafiki yake Ryan Giggs ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa Man united na mchezaji mwenzake aliyeko West Bromwvich, Darren Fletcher, huku kwa pamoja watatu hao walionekana kucheka na kufurahi wakiwa na mabingwa wa zamani wa mieleka wa WWE, kama John Bradfield na Layfield.


Muda mfupi baadae hali ya hewa ilibadilika baada ya Rooney kukaa na motto wake kai mwenye miaka sita baada ya Barrett kumdhihaki huku akiendelea kumdhihaki Ndipo mshambuliaji huyo akimzungumzia motto wake huku akidai hakufurahishwa akiopna akiwa amekaa kiti cha mbele, ndipo Rooney alipo nyanyuka na kumwendea Mwanamieleka huyo na kukabiliana nae ambapo alimpiga kofi usoni.

Lkini picha za marudio za video zili muonyesha Barrett ambae aliwahipia kuwa Bondia akimuendea Rooney na kuanza kumshambulia kitendo kilcho jibiwa na mwanasoka huyo udhalilishaji wa wazi.

Tuesday, November 10, 2015

Vifaa vya Judo kupigwa Mnada





Vifaa vya mchezo wa Judo vilivyotolewa na Shirikisho la mchezo huo Duniani IJF, viko hatarini kupigwa mnada baada ya chama cha Judo Tanzania  JATA, kushindwa kulipia ushuru ili kuvigomboa bandarini.



Akizungumziasakata hilo Katibu mkuu wa JATA, Innocent Malya amesema chama chake kimeshindwa kulipa ushuru ili kuvikomboa vifaa hivyo kutokana na changamoto mbalimbali na hivyo huenda vikapigwa mnada.



Malya alisema wakiamua kuwaambia ukweli JIF, kwamba wameshindwa kulipia ushuru ili vifaa virudishwa viliko toka  huenda waka vipeleka na hicho ndicho kikwazo kingine baada ya selikari kutaka vilipiwe deni wanalo daiwa ambapo IJF, ilisaidia kwa kutoa sh. milioni 3.6, na kilicho baki kilikuwa sh. milioni 9.2 ili viweze kutolewa.
Baadhi ya wanafunzi wa JUDO nchini Tanzania wakionyesha bendera ya Taifa.


Hata hivyom alisema kinacho elekea kutokea kinafanana na kilichowahi kufanyika mwaka 2006, ambapo JIF iltoa vifaa lakini vilikwama bandalini baada ya kukosekana kwa fedha za kulipia ushuru hatua iliyom sababisha vipigwe mnada.


Monday, November 2, 2015

Frances Cheka kuzichapa na Thomas Mashali


 Bondia mahiri, mwenye pumzi pindi awapo ulingoni Frances Cheka anatarajia kuzichapa na mpinzani wake wa jadi Thomas Mashari tarehe 25 mwezi huu huko Mji kasoro bahari Morogoro.


Pambano hilo ambalo litasindikizwa na pambano kati ya Mohamed Matumla a.k.a Matumla Jr na Mfaume Mfaume a.k.a Master, lakini pambano hili la kusindikiza litakuwa na upinzani mkubwa kutokana na kwamba Mfaume Mfaume alikuwa anamtafuta sana Mohamed Matumla, lakini Matumla Jr alikuwa akimkwepa.

 \

Mfaume Mfaume auzungumzia mchezo huo:
Bondia Mfaume, hayupo pichani ambae anashika nafasi ya tatu kwa ubora katika uzani wa kilo 63 kwa mabondia wa Tanzania wakiongozwa na bondia Twaha Kiduku, na kufuatiwa na Ibrahim Class a.k.a King Class Mawe. Ameweza kujinadi kuwa mchezo huo ataumaliza kwa Round tu


Amesema kwanza nashukuru tangia nimeanza mchezo huu nikiwa chini ya kocha wangu Rama Jah hadi sasa nimepigana mapambano tisa yasiyo ya Ubingwa na nimeshinda nane na kupoteza moja ambalo nilipigana na Cosmas Cheka.

Hata hivyo Mfaume alijinadi kuwa hadi sasa kuna mabondia baadhi wananikwepa kama Matumla Jr, na mwingine ni Cosmas Cheka ingawa awali alinipiga kwa pointi hivyo nawaambia wajipange kwa maana niko vizuri kwa sasa baada ya kunolew vya kutosha na kocha wangu Rama Jah na ninaaminim nitamchapa kwa round.

Monday, October 19, 2015

MABIGWA 5 KATIKA BURUDANI ZA MIELEKA DUNIANI, MWEZI WA 10/205

Kutokana na mechi mbalimbali katika World Wrestling Entertainments (WWE),zinazoendelea huko Marekani ndani ya mwaka huu 2015 katika mashinadano matano ambayo ni.


1. Wwe World Heavyweight Champion, Na bingwa wa Mkanda huu ni Seth Rollins ambapo kama unakumbuka Rollins aliweza kushinda mkanda hu wa Heavyweight pale ambapo Superstar Brock Lesnar na Roman Reings walipokuwa wakipigana na Seth kuingilia mwisho wa machi hiyo lakini kutokana na sheria za mchezo huo Seth aliweza kushinda. 
 
 2.  Intercontinetal Champion, na bingwa wa mkanda huu adi sasa ni Kevin Owens.



3. United State Champion, ambaye bingwa wa mkanda huu ni WWE Superstar John Cena.





4. Tag Team Champion, ambaye bigwa wa mkanda huu ni mpiganaji machachali Koff Kingston, 



5. Divas Champion, na bingwa wa mkanda huu ni mdada ambaye naye ni machachali sana anaitwa Charlotte,  shindano hili ni la wadada.


 Hawa ndiyo mabingwa ambao wanaendelea kushikilia mikanda hiyo yote ya World Wrestling Entertainments.